Matokeo Ya Usaili Ajira Za Umma 2025: Jinsi Ya Kuchukua Hatua Zako Baada Ya Uteuzi
Habari njema kwa waombaji kazi mbalimbali waliofanya usaili kati ya tarehe 02/09/2024 na 18/05/2025! Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma imetangaza matokeo ya usaili, na orodha kamili ya waliofaulu imechapishwa. Hii inajumuisha pia baadhi ya wasailiwa waliokuwa kwenye kanzidata (database) na wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana.
Nini Kifwata Baada ya Kufaulu Usaili?
Kwa wale wote waliofaulu usaili na kupangiwa vituo vya kazi, hatua inayofuata ni muhimu sana:
Pata Barua Yako ya Uteuzi: Barua zako za kupangiwa vituo vya kazi zitapatikana kupitia akaunti zako za Ajira Portal kwenye sehemu ya “My Applications”. Hakikisha unapakua na kutoa nakala (download and print) barua hizi.
Ripoti Kwenye Kituo cha Kazi: Unatakiwa kuripoti kwa Mwajiri katika muda ulioainishwa kwenye barua yako ya kupangiwa kituo cha kazi. Ni muhimu sana kuhakikisha unaripoti kwa wakati.
Nyaraka Muhimu za Kuambatisha: Wakati unaripoti, hakikisha una vyeti halisi (Original Certificates) vya masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea. Vyeti hivi vitahakikiwa na mwajiri kabla hujapewa barua ya Ajira.
Majina Yanayohusika na Tangazo Hili
Tangazo hili linajumuisha uteuzi katika Mamlaka mbalimbali za Ajira, ikiwemo:
- Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)
- Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
- Halmashauri ya Mji wa Bunda
- Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli
- Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
- Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma
Baadhi ya kada zilizoorodheshwa ni pamoja na:
- Laboratory Technician II (Fish Processing)
- Workshop Assistant II (Fitter Mechanics)
- Afisa Lishe Daraja La II
- Afisa Tehama Msaidizi Daraja La II
- Afisa Ugavi II
- Afisa Ununuzi Daraja La II
- Artisan II (Electrical)
- Artisan II (Plumbing and Pipe Fitting)
- ICT Technician II
- Instructor II (Mineral Processing)
- Instructor II (Mining Engineering)
- Instructor II (Theatre Art)
- Instructor II (Music)
- Janitor II
- Laboratory Assistant II (Embalmer)
- Laboratory Scientist II (Aquatic Sciences)
- Laboratory Technician II
- Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja La II (Records Management Assistant)
- Mtekinolojia Maabara II (Health Laboratory Technologist II)
- Mtekinolojia Msaidizi Daraja La II – Maabara
- Mwalimu Daraja La III B (Kiingereza, Shule ya Msingi, Uraia, Baiolojia, Kemia, Fizikia, Kilimo, Tehama)
- Afisa Afya Mazingira Msaidizi Daraja La II (Assistant Environmental Health Officer II)
- Afisa Ufugaji Nyuki Daraja La II (Bee-Keeping Officer II)
- Daktari wa Upasuaji wa Kinywa na Meno II (Dental Surgeon II)
- Tabibu wa Kinywa na Meno Daraja La II (Dental Therapist II)
- Afisa Kilimo Msaidizi Daraja La II (Agricultural Field Officer)
- Katibu wa Afya Daraja La II (Health Secretary II)
- Mtekinolojia Dawa Daraja II (Technologist Pharmacy II)
- Nursing Officer II
- Tabibu Daraja La II (Clinical Officer II)
- Administrative Officer II
- Afisa Maendeleo Ya Jamii Msaidizi Daraja La II
- Afisa Ustawi wa Jamii Msaidizi Daraja La II
- Afisa Utumishi Daraja La II (Human Resource Officer II)
- Fundi Sanifu Maabara ya Shule Daraja La II (School Laboratory Technician II)
- Mwalimu Daraja La III C (Hisabati, Historia, Tehama)
- Afisa Hesabu Daraja La II (Accounts Officer II)
- Afisa Kilimo Daraja La II (Agricultural Officer II)
- Afisa Kilimo Msaidizi Daraja La III (Agriculture Field Officer III)
- Msanifu Majengo Daraja La II (Architect II)
- Forest Officer II
- Mchumi Daraja La II (Economist II)
- Mtakamu Daraja La II (Statistician II)
- Planning Officer II
Kwa Wale Ambao Hawakufaulu
Kwa wale ambao majina yao hayapo katika tangazo hili, mjue kuwa hawakupata nafasi au hawakufaulu usaili. Hata hivyo, msisite kuomba tena nafasi za kazi zitakapotangazwa.
Hongera sana kwa waliofaulu! Hiki ni hatua kubwa katika safari yenu ya utumishi wa umma.
Tagged: News