Maandalizi ya muhtasari wa Elimu ya Msingi Darasa la I na la II yamehusisha wataalamu mbalimbali kutoka taasisi za serikalina zisizo za serikali.Taasisi ya Elimu Tanzania (TET),inatambua na kuthamini michango ya washiriki wote waliofanikishakupatikana kwa muhtasari huu.Aidha,TET inatoa shukurani za pekee kwa wahadhiri,wakufunzi,wathibiti ubora wa shule,walimu pamoja na wakuza mitaala.Vilevile,TET inaishukuru Kamati ya Kitaifa ya Wataalamu ya Kusimamia Kazi ya Maboreshoya Mitaala ya Elimu ya Awali,Msingi,Sekondari na Ualimu iliyoteuliwa na Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia.Kamatihii ilifanya kazi kwa weledi na kuhakikisha kuwa maudhui ya muhtasari huu yanalenga kuwa na wahitimu wenye maarifa,ujuzina stadi zitakazowawezesha kujiajiri,kuajiriwa na kumudu maisha yao ya kila siku,ambalo ndilo lengo kuu la Uboreshaji waMitaala ya Mwaka 2023
ATTACHED FILESFile | Action |
---|---|
muhtasari-I-na-II.pdf | Download |